STORY – Eastland Gold by Mwas Mahugu (Sheng language, fiction)

(read Mwas Mahugu’s interview, poems, and check out some of his lyrics)

NOTE: This piece is an excerpt from a work in progress.

gas fence


Synopsis.

RAGS TO RICHES, OF A GHETTO BOY AND BUSINESS RIVARLY WITH TWIN BROTHER, ENVY, LUST, FAMILY FEUD, STREET GANGS, FAILURE, SUCCESS. LOVE AND HATE/CONFORMITY/REBELLION.

ksh1k

K- town ilikua imetulia sana especially ka ulikua umetoka the other side of the town,kaa ungetaka kurejuvinate mind,kupata ile inner calm yak u-enjoy nature,basi hii ingekua your perfect escape,ni vile tuu sometimes kulikua frequent gun exchange ya makarao na madingo,hizi streets exchange zilikua fun kwa watoto wa primo,since chuo zikifungungwa walikua na version tofauti ya “Godi sinya”walikua wanamake gun za wire,na rubber bands,na whole day ilikua ni cat and mouse kwa alleys za k-town,naughty boys sometimes wange shoot buttocks za wamatha,games zilikua mob taya,bano,cattie,
Watoi machokosh ndio tuu walikua washajua hustle before,walispend the whole day waki collect carton peppers,plastic,machupa,na ma-srcap metal..sometimes watoi wa estate wange simamisha game zao za guns za wire,na ku scream in unison “”chokora mapipa chokora mapipa”na immediately tu-wars tulikua tunaanza,wakishoot.but ma chokosh walikua wan give up juu always walikua-anga super dupa high na chupa ya glue,lower lip ilikua ina suspend na kushikilia hii,hata mbio gani hainge fall.
Street za kuinfia k-town zilikua za nguvu, artificial flowers za miscellaneous colors,zimepangwa all overna design ya abstractna ma officious,hawa wasee walikua wameadvice raiya kumwaga soil kwa hizi roadii za mtaa ili kufunika lami,solar ikiwa hot lami ilikua inachoma watoi miguu wakiride ma-tyres,hii issue ilikua inaleta ma-paroo juu:reason being after mtoi ku-burn na lami alikua anarudi home na statement kaa hizi zilikua za kawaida””aaahhh woishe Mama nivae viatu za shule leo pekee?”nimechomeka sana
‘’’NGRRRRi krriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiing bell na ilimalaizia
Watoi wli-ignore bell na kundelea kuchaza ball ya ma-paper,ilikua ni break time ya afternoon,kitu 4pm,middle classes zilikua zishagoo home,na maboi walikua wajibamba,moodee yani mwalimu alitokea from no where!
“Hey boys it is time to go home,play time is over go home.teacher alli-annouce loudly
Tonii ana grab ball speed speedie na bila kerespond anatoka teke teke akifuatwa na ma-boys wengine.
Teacher naye anahead back kwa classes,k town primary school,imejengwa poa,concrete walls na roofing ya grey asbestos ilikua chuo ya nguvu.
After dakika kadhaa Odhis wali slow down after kupenya kwa mtaa,walikua wana hema sana juu bag heavy juu ya books.
Toni:Manze jo mo-dee amekatisia game mbaya
Beste: Toni manze nilikupiga chobo!! Ha ha ha
Toni:na nani? Nani? Sura ka chobo!! Ha ha
Beste: umenza mchongoano?
Beste 2:kaende kaende mimi ndio refa,boi mwingine wa tatu alichangia
Soon walisimama na kuform a circle na mchongoano ikaanza.

Sky ilikua radiant ,miale the solar zilikua zinaptia hii golden rusty color ya nguvu,wasee wa kupika mandazi , walikua wanarudi bizness round two!fishmongers,mutura ,supu,nyam chom round ya kwanza, waki wxpect booming business ,wasee wakitoka job,wna watoi wakirudi home kutoka chuo,jamaa wa ice cream alikua busy whole day,
Msee wa kuuza miwa alipita, na baba Toni aka mwita,
“tukatie na utu chongee ya 20 bob”na ugawanyishe mara mbili,baba toni ali show msee wa miwa.
Baba toni.: rafiki mambo yamekua magumu, (alisema huku aki clear throat)
Jirani:Si kwako tuu,ni kila pahali,ni kawaida ya maisha
Baba toni:hata siamini ni huyu motto wangu toni<
Jirani: amefanya nini tena?
Baba Toni:ana bidiiii sana shuleni,tabia nzuri naomba mola nihakikishe amefika chuo kikuu rafiki!

Trader wa kuuza miwa ana maliza kuchonga miwa na ana pass kwa Baba toni na rafiki yake,but wote wanapatwa na surprise ,
“Hata mimi na taka miwa baba,Toni anadai huku amebeba bag na paper bag kwa mkono.
Baba toni:haya mchongee ya 10 bob anamwambia msee wa miwa,hukua akimgeukia motto wake toni
“umetoka wapi?usiniambie tena pia umeokaota okota hivyo vyuma?aaaha?
Toni:mbuyu unajua tumesota,mee nita uuza hizi tupate za chakula ,na wewe ulipe karo
Baba Toni(defeated)basi ingia ndani wenzako wako ndani
Aha ha ha jirani anacheka kidogo “watoto wa siku hizi!
Baba Toni :wamuona weekend zote hushinda akiokota hivyo vyuma juu hakuna shule
Jirani:atakua mtu wa heshim a kwa jamii,sio kama hawa!una waona,:jirani ana-point jamaa wawili wanapita street wakistagger, “wamesomeshwa halafu baada ya hiyo bidii yote na pesa matokeo ndiyo haya”!
Baba Toni:muone hata hana haya ana kojoa hadharani!
Drunkard wa pili pia ana move kwa wall na pia kunyoraa,without giving a damn.

Crow ikoo juu ya green street light ime spoil,malibou stock ziko juu ya mitii mbili zilio kwa hii street,na pia kuna moja ina hop hapa na pale,ina limp.ni non approved refuse pit next kwa stage,ma bachelor na wasee wakurauka ngware ndio course ya excistance yah ii site,huanza one paper bag ,siku ya pili two,na soon ,kila mtu wakurauka job early ana follow na uchafu yake na soon after,uchafu kupile up.pia mchana hakun a ana aibu ya kutupa hadharani.
Toni anascavange for scrap metals na ma-plastic,kwa hii dump pit,anavunja upande wa kushoto na achecki original street Boy aki approach
Street boy 1,tulikwambia hii si job ya wasee wako chuooo,weee ruudii shuuule!
Street boy2:first leta hiizii .
Street boy anamnyang’anya Toni collection yake,huku toni aki-refuse
Aaaaaaaaachilia chokosh wapilia anadai huku aki mshika kidevu,Toni ana-fall,na machokosh wanatoka teke teke

After sometimes,malibou stock ina shonde kwa face ya toni ,na hako ka baridi kan mrudisha kwa consciousness yake,ana walk home mdogo mdogo,huku akibreed kwa lips kiasi,
Bell yam see wakuza maziwa ya brookside,inamrudisha kwa flash back,hio incident ili-happen akiwa eleven years,3 years ago,na sasa alikua fourteen years na candindate,Toni alikua ame lean kwa wall behind class eight classes,
On the front side,ni celebration,pupils washikilia exams pads na geometicals sets,hewa imejjaa happy voices na murmurs,jumping up and down,hugs na kisses,wote wana celebrate Kumaaliza Kenya certificate of primary education(KCPE)exams
Toni ana-wajoin lakin I amevaa sura ya kazi
Pupil:checkini huyu msee(all attentions kwa toni as murmurs zinadie)
Pupil 2:sura ya kazi ya nini?shida ya nini?
Pupil mwingine anatokelezea na teje boom box ya nguvu huku ame I carry kwa shoulder,attention ina leave Toni
Boi:Ha ha ha Njoro umechukua teje ya home kwenu?kichwa yako mbaya!
Njoro: hei hei msee wangu kua mpole nina ma- mix mwenda after all exams zimekatika

Ana switch on teje “ a big tuuuunnnee,pfhooo… a horn blast, DJ bunduki on the mix!”the rough and toughest this is followed by a raggaa riddim,and everyone is dancing.inabidi madame wainue skirk kidogo hadi kwa knees ndio waweze kuziondoka,na kila boi alishikilia manzi kutoka nyuma.

The same Dj mixx inaendelea kuchuna kwa matatu,raia ni wengine ,horns za magari kila pahali,makarao,ma-hawker, mabroker,ma-hustla ,ma-sonko,Toni anauza njugu.
“nani mwingine?nani mwingine?
Mara msee anamvuta kutoka nyuma!raia ni ku-stare tuu kawaida ya Nairobi
Stranger: we fala nani alikua mbia unaweza uzia jugu hapa?ana uliza kwa ukali
Toni:ati nini kaa huna doe ishia!toni anajibu kwa ukali
Stranger na –moove next na Toni kumushika masharti na kumkaribia kwa face,pia boi mwingine anajoin na soon Toni ako surrounded,msee mmoja anachukua juguu tano,
Na ku-point toni “wee fala na uchunge line zetu
Toni:fala ni wewe na ulete doe ya juguu,tusi zoeane.
Mara ngumi heavy ina mpata Toni,ikifuatiliwa na ingine kwa kahasho,Njugu zina fly kwa hewa na toni hajui kaa anaona njugu ama nyota…….

gas spraypaint


Chapter two

Baba toni ameshikilia gazeti,aki chill food,na kwa korner ingine ya room Mama toni analeta plate ya tilapia fish na ugali,kama kawaida inawekelewa kwa table sister na bro wa Toni wako wana-salivate.
Baba Toni.kila siku samaki ugali,kila siku samaki ugali!kwani majirani wamekufunza nini?
Mama Toni:kwanza samaki in demand sana tafuta pesa ufungue kibanda,wacha maneno ya kutafuta kazi..hujui hakuna kazi baba
Baba toni:pesa ziko wapi?mama watoto,Toni huyo ana faa a join form one
Mama toni:lakini baba watoto si wale watu wa NGO wanalipa karo
Baba toni,wanalipa 80% na sisi 20 % na tununue uniform!
Mama Toni:usijali mungu atatuonekani.
Family ya baba toni ilikua na watoto watatu,vijana wawili na msichana mdogo,Timo alikua ameachwa na miaka tano na Toni,Toni alikua 15 years old,na ready kujoin form one,maparent wake walikua proud na biidii yake especially after Kcpe,Toni alikua a young hawker in Nairobi town,hii bidii ndio ili-attract mama toni kwa Baba toni,but nowadays mama toni alikua ashaboeka na Bwana yakee,juu alikua asha kua m-lazy,alichunjwa job,5 years ago na akaukua alcoholic,na ku-loose any drive ya creativity na pia morale ya kusaka job.Baba tony alikua na ana leave in denial na pipe dreams,za kurudi job kwa Samken logistics kama machine operator,Mama Tony alikua ashachoka na version yake ya reason ya kuchunjwa job,Baba toni alikua ana dai eti alikologewa na kutupiwa majuju,na workmates wake,but the heart of the matter kampuni zilikua zina streamline workers,juu ya hard financial times.
Mama Tony ndiye alikua bread winner pekee ,alikua ana uuza second hands clothes gikomba,but off late alikua proud of his son Toni juu ya back up,from his hawking business.how ali-wish twin yake angekua.alikua ana leave na regrets za kupatiana one of the boy to adoption.but hakua na choice,walikua so broke na jobless fifteen years ago,na walikua wanaishi Koch shanties,nyumba za matope ,na mabati za drum,although hawakua wame piga progress sana but now ,walikua wanaishi kwa plot nyumba yam awe na toilet walikua wanashare na wasee wengine saba,kwa bafu ama toilets asubuhi ndio the only way ungejua majirani,juu sometimes walikua wana patina hapo,na ilibidii ku-que In turns,so they all knew Yule msee akiingia toilet mbele yako,ni mambo badd ,juu kuna wasee walikua wan dung asana,pia hii area ya toilet na bafu ndio ilikua place ya kufulia na pia,platform ya mpango wa kando,amenities zote communial ,zilikua hapa pia sink,zote zilikua mwisho ya plot.
Kulikua na siri za kila plot,nani hu hanya nani?nana hupiga wife usiku,mlevi na pia nani ameokoka,most Fridays kulikua na Jumuiya wa wakristo,na wasee wa church wangekuja kwa mama Toni ,kwa maombi,times kama hizi .Baba Toni alikua missing na ungempata Kahuruko basa,akinywa barley na wazee wenzake,wote walikua na same stories vile walikua na pesa kitambo,before shetani atokee kwa life zao.
Nyumba ya family hii,ilikua one room,na kulikwa na curtain imegawanyisha keja mara mbili,Toni alikua akilala kwa sofa na wataoi wengine waliktandikiwa chini,for the last 3 years sex life yao ilikua affected sana since,mama Toni felt,Toni was a young adolescent man,and so alikua amechill,but the real truth was since Baba Tonni aingilie pombe,alikua asha kua one minute man na time mob,Mama Toni alichwa hanging’but alikua asha jipanga na bwana wa jirani,so waliishi hivyo.naye Baba Toni alikua ana pata service kutoka kwa Bar maid wa kahuruko,according to rumors kutoka kwa wamama mabeste wa mama Toni,zilisema pia Baba Toni ndiye alikua analipia Bar maid waithera nyumba,but since Baba toni amu slap ones alipoenda kumake enquiries ,3 years ago,She shut up,na akatafuta mpango wa kando.although alikua ana feel guilty kila siku,na alikua ana ogopa watoto wajue..
Mara mingi scandles za mapenzi zili-kua zina fichuliwa na watoto wakichongoana innocently
“Wee nyamaza na mama yako hukuja hukuja kudowea food kwetu”wakati mama ametoka once a neighbor son told Toni 4 years ago,but luckily hakukua na watu kwa plot.

Toni ali amka huku amechangayikiwa,aliokota njugu zake,akirudisha kwa basin but mob zilikua zishakanyagwan na raia,mara askari wa Kanjo akatokea,na ku-knock Tony na boots zake
Askari:wewe nyanga’u unafanya sarakasi gani hapa?
“Nimepigwa na wakora ‘Toni alijitetea
Askari:wakora wagani ?amka kwenda nyumbani,ama nikutupe kwa lorry,wewe ni motto mdogo
The council askari alim-slap kwa mgongo,Na Toni alisahau njugu zake na kupotea mbio,alikua ashasikia story za kufungiwa juu ya hawking,Toni alishika njia ya river roadi ndio atelemke Otc achukua mat,after dakika kadhaa,one hundred metre ndio afike kwa stage yake,alishangaa watu walikua wakiscream all over ,loud bangs za milango za business zikifungwa,carn horns, mara smoke ikajaa kwa hewa,haikuchukua time mob before Toni ajue ni Tear gas ,alikimbia Nduki,na kuchukua alley tofauti,hakua ana ona vizuri and was everyboy marsa kwa mara kulikua alingona na watu,but ilikua ni Kiguu ni ponye.
Hali ya taharuki ilikua ishajitangaza,watu wakikimbia kila place,Toni ali slow down!
Kando ya road mwanaume alikua amelala chini,in seconds kila mtu alikua akisimama kidogo na kundelea kukimbia,damu ilikua itiririka kutoka kwa mguu,Toni alizubaa kiasi but network ku-rudi na reality,ali run na kundandia matatu,alipata seat next na mzee flani.na kutry ku-relax.
Huyo mwanaume ni mwizi..mzee aliuliza
“Sijui,Toni alijibu
“amekufa ? sauti ingine iliuliza
“Nadhani “toni alijibu huku akipumua
“wacha wakufe hawa wezi ndio wana tuhangaisha usiku”sauti ya manze ilichangia kutoka back seat.
“ameiba nini?mama alikua kiti mbele aliuliza
“eti mkate!sauti ya mzee nyuma yetu
“ wacheni fitina mimi nime ona na macho yangu ,alikua hawker amenuizia kitambaa,dakika chache kabla city council askari wampige! Huyo sio mwizi,mama alikua na machungu na huruma aliongea.

Conversation zikaanza,na soon kila msee akaanza kupeana version yake,hata walevi walichangia, after kuchoka,kila mtu akanyamaza,after time music sytem ikaashwa
Feeling na atmosphere ina change,viti niza velvet ,graffiti na portraits za mean face black American stars zina ni stare nika tuna-beef bado!
…Noma noma..noma riddim flani ya ragga ina –blast kutoka kwa ma –woofer,macho zote za passenger ziko glued kwa plasma screen,scenario ni palms trees,aqua blues sky kwa background,Jamaican Artistes ndio main attraction,but kwa side show,kuna scantly dressed ladies na ma-bikini.
, unexpected abrupt breaks ,hu-ku-force ukae sober,hakuna cha day dreaming kwa Nganya,nikushikilia ile kiti iko mbele na mikono miliwi,otherwise kichwa yako itagonga ceiling ya mat,na impact ya kurudi kwa kiti pia ,inaumiza especially ka mathutha zako hazina enough shocks absorbers,
madere hawana huruma,na pia sikupenda kwao idhaa haiwarusu.ni paper chase,na kwa roads za Nairobi wana rule,ku-break rules nikawaida ka macho ku-blink,ku-break rules ndio law,Matatu ina stop abruptly, suddenly policeman amevaa sura ya kazi anaingia na ku-uangalia,kila mtu amenyamaza,ngoma ilizimwa kitambo.
We conductor wapi kiti yako?
Koni-kodi anamvunjia na design flani,karao anashuka,na conductor anamfuata nyuma,after dakika mbili,kuna loud banging ,simultaneously mat ina-move,
Vj a.k.aDj kalonje ndio ako on the wheels of steel ,ngoma inarudi ka kawaida.entertainment full blast,woofer zinachuna karibu zi-blow heart ya msee injebaada ya muda ,
Toni alishuka matatu, na ku-ingia mtaa wa K-town,watu walikua wengi na pia biashara za jioni zilikua mob,music hawkers walikua busy na Tv zao kwa street wakuiza cds na movies na Dvd,wamatha walikua wakikatia watu mboga kwa kiosk,harufu ya fried fish na burnt animal fat ilikua all over,
k-town usiku giza ilikua totoro,murmurs ndio zilikua kibao,once in a while unge-nywesiwa na bike,ya ma-milk vendors waki deliver maziwa ama mikate,butchery zilikua na customers na pia ma-shop,but watu walikua busy ilikua wasee wa kuuza mutura ,maini, na soup,so among the murmurs sounds ilkua ina sikika sana ni ya msee wa soup aki-i-beat kwa kibuyu,clad na white dust cost ,
Once in a while ungesikia ma-nduru uki –walk kwa hizi street,most def ilikua ni either ka -newborn baby amewasili..Story za hosi zilikua ni fyam.hakukua na dawa,juu zote zilikua zishauzwa kwa ma-phamancy za mtaa,pia story ya the famous pastor Deya ilikua inachangia sana..Ku-delivier kwa hosi chances za mtoi wako ange disappear miraculously zilikua high sana.
Nduru ya pili :ungesikia kwa same street ni ya msee akipigwa touch!yani ngeta kwa ufupi,ka-evening rush ka mabuda kupeleka kwa nyama quarter home baada ya kuangusha tu-kilo kadhaa na mabuda wenzake..ilikua ni celebration kwa petty thieves wa K-town .sana sana walikua ni walevi na sometimes sober,vitu zilikua zina move fast. kwa hii street unge-checki nyuma ama sides just ku-make sure your ass is not the next one on-line,hii ilikua street reflex, hata ka ni gun shot zilikua kwa hewa..kila kitu ilikua ni kawaida no big deal,although resident walikua wanatoa tax kwa self appointed community policing,kulikua thin line between ma-dingo na security.

Nduru ya tatu: ilikua ya any body .admist hizi fracas Makarao walikua wana- supply mwangaza for a while.but resident walikua wana pay heavily for the light.mataa ya ndai ilikua always full light,ilikua ina-stand far,ma boi wa kiganjo..Maboi wa murungaru..Kwekwe.. Spider.. ma-beast..mambang’a e.t.c names zilikua endless,walikua wana ndondoka na ku-spread huku waki –ji-mix na raia.so nduru yetu ya tatu ilkua ni ki-bare ama kama huelewi na maanisha kofi.either ya kijana amepatikana na twenty bob kwa mfuke pekee yake,ama ya mother alikua amekuja kutetea motto wake
Mama “mnashikia Kijana wangu nini, nime memtuma kwa duka tuu saa hii!
Mbang’a “ twaaafff! Ki-balee ya nguvu!) mama tunamjua mtoto wako,ni jambasi tumemtafuta sana”
scenario kaa the only option ilikua nu ku-rush kwa mattress account ama akope-Wamercy.soe moja ili mtoi wake aachiliwe.every resident alikua vulnerable ku-transformiwa pesa point kwa hako kagiza.pingu ndio ilikua A.T.M card.
Nduru ya inne: ilikua lovely.all roads after hizo drama zote zilikua zina lead to of course kejani. Plot zilikua zimeshikana bampa kwa bampa some za ngoro yani high rise.every plot ilikua na approximate watu fifteen, so ka ni ngoro una multiply,although Country yote ilikua na receive heavy rain downpour,still power rationing zilikua ni zaa kawaida ka oxygen,rationing ingeisha aje,na ma-Minister ama ma- Mps, ndio walikua wanauzia Ken Gen power. Generators za kutumia diesel ndio zilikua zina churn electricity,but according to officios report,a foreing company ndio ilikua imepewa tender..ili ku-ease rationing,for all those years hata after LA-Nina Na EL nino ku-come hatu-ja-wasikia rationing zimeisha.so back kwa nduru yetu ya nne,
ilikua nyuma ya ma-candle lit dinners,after-ku- watch news..ya the same same boring Leaders with same same old script. anglo leasing, golden berg.maize scam triniton deals a scandals ,Citizen protest,l ast but not least KCC ikimwaga Thousands litres of milk,ka-ghetto queen ange serve buda,na ku-take position watching South american soaps ama Nigeria movies,after hapo ni slumber land.soo kwa –meda sometimes ilikua inanza early.ma-lovi davy..Dear I am coming..Ooo
Scenario ilikua the same Koinange street,but on that side ilikua ni between city officios, perverts and thieves in such of pleasures versus thigh-land squad caught up kwa paper chase ili walipe bills,raising children ama colleges fees.na usisahau Sunday morning church service hii squad ndio walikua may be biggest contributors, to the coffers.just a may be!

Toni alifika alifika kwa plot haikua imefungwa main gate nakingia nyumbani kitu saa nne.
Baba toni:habari ya kushinda mwanangu?
Toni :poa mbuyu
Mama toni :biashara vp?ali uliza proudly
Toni:karao wa kanjo mama
Wazazi waliangaliana,na toni akawa angalia kimya chake kili sema yote,hawakutaka mengi juu haikua siku ya kwanza.
Mama Toni:mwanangu chakula hicho hapo,sisi twaingia kitandani
Baba toni alimfuata wife.na wazazi wakingia nyuma ya curtain,palipo kua na kitanda.
Mama toni:ukimaliza asha mosquito coil,na usisahau kuzima stima
Toni :sawa mama
Toni ali ji serve food ,na akashangaa bro yake alikua amekondoa macho haja lala
“Wewe timo watoto wa rika yako wadooze”una wait nini?
“Umeniletea nini Toni?” timo ali –ask na whisper
Mama toni:Timo huja lala nikishuka utanijua,na wee Tony uamke mapema chukua pesa hapo chini ya radio,uende gikomba mapema ununue sanduku,tunaenda shule boarding kesho.
Timo alifinyia bro yake macho na kujifunika ,sara sista yake alikua next nay eye,na alikua slumberland aking’orota.baada ya nusu saa,Toni ali asha candle akazima stima,akazima radio,na kudooze.
Morning K-town ilikua radiant,clear sky na patches za clouds hapa na pale,watoi busy wakienda chuo ,mama mbogas wakirudi kutoka soko,raia ya industrial area,jeshi mathree taking over the street,pia wasee wa kurauka kwa vichinjio,Daggoreti.Njiru,Kiamaiko,na Burma pia wako budy na bike ama gari zao za color red na black,wote wako njiani yani wote wote wako kwa streets, Civil servants, Doctors, lawyers ,entrepreneurs, hawkers, street preachers, con artist, real artist wote wame-rise early in the name of national building,residents ama citizens wa dee phase ni hard working sana.
Tony alirauka ngware na kueleka kwa stage,soon matatu ilikuja
“Evereday day am hustling,This is Hepta entertainment….Dj mantrix on the mix .Plasma screen illi-annouce loud and clear.Air fresh ya perfume ili pata Timo ku-checki side alipata smile na alikua wa-power,
Timo: “sasa unaenda wapi ?asubuhi hii!
Msichana: “Nani amekuambia nataka kubonga na wewe?
Timo “Oohh pole!ali-apologise
“narudi kwetu na enda shule kesho ”alisema na kunyamaza
“umeitwa shule gani?Timo aliuliza
Alivunjia Timo kutoka kwa kiatu hadi kichwani alafu reluctantly ,
“unaitwa nani na unataka nini?
‘Timo” alisema
“mr Timo naitwa suzy na sitaki story mob,sawa?xaxa ni saa ngapi?ni mapema sana.

Timo ali –give up,na kuendelea kuangalia inje na soon,matatu ilipata huruma,air force,na ikafika eastleigh.
Matatu na magraffitti,majiana kali kali ka,Field marshal Kimathi,street soldiers,rebel ,Harlem,mafia squand,black militias,street theatres,watu ka siafu waki –kriss cross street,mabuda na ma-kanzu,wamatha na bui bui,mashory na hipsters machali na hoods,ilikua ndio sight.scent kwa hewa ilikua tamu tamu ya biriani ,spices kutoka kila corners,clothing ,perfumes ,electronic shops zilikua dominant,sound kwa hewa ilikua horns za number tisa,na kutoka kwa loud speaker.za traders,just like dee phase resident wa huku walikua hard working sana,but the same officio cartel activities zilikua dorminat hapa.un collected garbage all over even next to a military air base camp,roads zimejaa pot holes,
Jua ilikua pia ina take position kwa sky,ma-doves kibao zili-fly na ku-stand kwa wire ya stima,mat ilipita main road past Mater hospital,Eastleigh,every side ilikua na state of art shopping malls na pia ,kulikua na mosque biggie hiyo area.
Matatu ilipita California,na baadaye ikafika Gikomba Open air Market.As early as nine morning,kuna preacher ana preach akimove to and fro distance ya fifty metres,side zote ni highrise vendors,waki arrange merchedise wares zao,,
“Habari mathee”timo alisalimiana
“Sema
“ nikuzie nini?
“Nitaka sanduku ya shule
Vendor: Karibu mwanangu unataka gani?
Anachecki checki na ku-point moja
Hii ni pesa ngapi?
Vendor: Mia nane baba
“Mimi nina mia sita”
Vendor: Ongeza mia baba
“Sina’
Vendor: Ulipewa ngapi na Baba
“Nilipewa mia sita na mama,tafadhali nuizie hivo sina haki sina”,
Vendor:Sawa baba leta,we we ni motto wangu
Timothy Karanja alinunua box ya blue,na akaweza ku-save mia tatu,mamake alikua amempatia mia tisa,alirudi nyumbani na mamak akampeleka jenga hekima high school,huko aliendelea kusoma ,huku akipendwa na wanafunzi na waalimu,by the time afike form alikua assistant school captain,na form four akiwa kaa skool captain aliongoza shule,kwa busara,na matokeo ya lipo tokea ya a mtihani wa KENYA CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION(KCSE)
Mama yake alikua proud sana akiwambia wenzake ,mwanawe alikua kati ya wale wanafunzi wali perform poa nchini kote,na pia moja ya bank ilikua ready kungalamia masomo yake yote.by this time Baba Timo alikua asha mwoa Waithera,na kuhama nyumbani,mama toni alijikaza kisabuni na wanawe,na success yao yoyote ilikua sweet kwa soul yake.
Young man Timothy aliendelea kusaidia mamake Biashara na soon ikapanuka kwa muda mfupi sana,masomo pia alitia biidii katika chuo kikuu huku akijihusisha na biashara..alitembelea Benki Ya equity na kupata mkopo,na akkaweza kufungua nduka la kuuza nguo mpya katika street ya Kimathi mjini Nairobi..Hiyo ndiyo hadithi.ama kama hujani pata story ya before ya Mr Tony Karanja,mwana biashara mashuhuri,mwenye timclads wear moi avenue,tim electronics ltd, Tony electronics,na mumiliki wa mother&son boutique

Bwana Tony alikua amespend two hours akifanyisha watu interviews,aka shortlist wawili,carol akinyi,na Jacob Mutua.timo aliamua kuanza na carol,alifungua makratasi yake,na kumkaribisha kwa offisi

Master of Business Administration Periyar University
Post graduate accounting
Followed by other a list of other qualificatios
From primary school alikua student wa straight A’s
“sista hii university iko wapi?Timothy ali ask
“Iko India,siku-manage kupata job huko juu sikua najua ku-speak ki-indree”carol replied
“na una survive aje huku Nairobi?Timo akauliza
Mimi hutengeneza liquid soaps na kuuza kwa plots,hotels ,shules na sometimes hospitals..sista ali- explain.
“okay umenifurahisha sana kesho report kazini”,
“oooohhhhwwwiii Carol alijump “asante”ali whisper.
Baadaye alifuatwa na bwana Mutua
Master Bs economics
Finance
Egerton University.
“bwana Mutua umenifurahisha sana,tupatane kesho for lunch,nitakuambia tuta saidiana vipi.timothy ali mwambia
“Asante sana bwana Tim,nitafurahia kufanya kazi na wewe”/ Mutua alisema……….

gas6


Middle chapter

Kila mtu alikua quiet,once in a while ,moving air ilikua inpata way na ku-blow nywele za ladies,na immediately Yule alikua kwa window,ange slid close window baada ya ka-upepo,kupunguza joto kiasi,time zingene nywele zao zinge-stand for an eternal moment, hii ilikua especially,time dere ange carelessly overtake ndai zingine,ama ndai ilipo hit a unnoticed hollow kwa hii Mombasa road,there was no reason ya sound system,of all the people kwa hii van Timothy ali notice wasee watatu alikua ana fahamu poa,wawili walikua cartel ya officio,but aliendelea kusoma gazeti.

Once in a while the resident would watch on television how the local government,had come up,with projects:poverty eradication,kazi kwa vijana,kick malaria out of town,hii ilikua followed na convoy of 22 tyres lorries,ziki-blast poverty eradication.ama stop drugs messages,luckily artist mmoja wa hizi town alikua na chance yak u-perfom,alafu jioni kwa news,wakaazi wa sekta town,dee phase,na k-town “wafaaidika kwa mradi wa serikali na NGOs.but zote zilikua zina exist kwa gazeti radio na Tv,but in reality ilikua ni uongo tupu,mara kwa mara wakaazi walimchagua mjumbe ,lakini baada ya kupatana na city officio mjumbe alibadirisha tabia zake ka kinyonga na kujiunga na city officio,grand corruption, poverty na mismanagement of fund.ndio ili wafanya ma alley cats kuanza kushika kipaza,na kuwapatia ujumbee wakaazi,bada ya moto kuwaka sana ,na kuwa choma ma officios.ma-city officio,walianza kutoka teke teke,na meza zikaanza kugeuka,hapo ndipo Mr Baba yao na mrs Mama yao,alianza kuonekena kwa street,na kitu funny,ni vile aliiga tabia za city officios.miradi ya kusaidia na sauti ya kumtoa nyoka pangoni…alimwaga pea nuts hapa na pale.na wakaazi wakaanza kumuita rangi ya pesa.

‘ukikataa utaniumiza kukupenda sitaweza”
Unanielewa mbona unachelewa mbona”
Niambie nije nije sasa hivi”
Song ya mbongo flava ilikua inachuna kutoka kwa streo speakers mdogo mdogo,place yenyewe ilikua imetulia sana,murmurs na whisper ndio ilikua code za conversation,café dela crème ilikua joint new Moi Avenue ,perfect haven ya raia ya middle class,haikua na swagg mob ka the rest za uptown,wasee hapa walikua less complex and real.
Tony hakua ameachwa nyuma ,na hio ndio place wali-have first date ,na ilim-take mbaya,within mwezi moja alikua ashaanua Suzzy,na kupiga rubber stamp.
Ali inua mkono na kuitisha expresso double,ya pilli,alikua asha kaa one hour waiting in vain,Suzzy alikua time keeper mbaya,Tony alishangaa.alijipa shughuli na kuanza kuangalia abstract [icture kali zilikua kwa wall,halafu aka-decide ku-log kwa facebook,alichomoa Tablet phone,aka –login na kuhit Suzzy kwa facebbook,

gas4

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s